Video
maarufu ya dansi ya mazishi ya wabeba jeneza wa Ghana ‘Coffin Dance’
imeripotiwa kupigwa mnada na kuuzwa kama mali ya kidigitali kwa dola
milioni moja.
Nusu ya mapato ya video hiyo ambayo ilisambaa kwa
kasi mitandaoni wakati wa janga la Covid-19 yataenda kwenye mashirika
ya kutoa misaada ya Kiukreni wakati wa vita.
Video hiyo
ilisambaa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2017 baada ya kuangazia
nyimbo na dansi zao wakati wa kubeba masanduku ya miili katika ibada
ya mwisho ya mazishi.
Na mwaka 2020, ilipata umaarufu
zaidi baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kuchukua dansi za
kikundi hicho kuleta mzaha wakati wa janga hilo.
Video hiyo imeuzwa kwa kampuni ya kurekodi muziki ya Dubai ya 3FMusic Aprili 9, 2022.