Waziri
wa Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy
Gwajima, amesema Serikali inaendelea kuwasaka wanajamii wanaofanya
matukio ya ukatili na unyanyasaji kwa watoto na kupelekea kukimbilia
mtaani na kuacha makazi yao.
Dkt.Gwajima amesema hayo wakati akiongoza shughuli za mazishi ya kijana Edik Gang'ata aliyechomwa kisu na kijana mwenzake mtaani,wakati kijano huyo akijaribu kupigania haki za vijana wadogo wanaoishi mtaani jijini Dodoma.
"katika zoezi la kuwafikia na kuwanusuru watoto wa mitaani linaendelea hapa mkoani dododma hatua kwa hatua na linaendelea kwenye mikoa mingine yote,Ndugu wananchi na wafiwa tukio hili la kusikitisha linatufundisha kuwa ndoto za watoto wengi zinapotea tangu wakiwa watoto"amesema Dkt Gwajima.