Bunge la Tanzania limemchagua Dk Tulia Ackson kuwa spika wa bunge hilo.
Dk Tulia amefanikiwa kuwagaragaza wagombea wenzake nane wanaotoka vyama vyengine vya kisiasa.
Tulia amepata jumla ya kura 376 kati ya kura zote zilizopigwa.
Tulia aliwahi kuwa naibu Spika chini ya aliyekuwa Spika wa bunge hilo Job Ndugai ambae amejiuzulu mapema mwezi Januari baada ya kutokea kwa mkwaruzano kati yake na rais.