Rais Kenyatta Kufanya Mkutano wa PG na Wabunge wa Jubilee Ikulu Leo.

Rais Uhuru Kenyatta hii leo ataanza kikao cha siku mbili na wabunge wa Jubilee katika Ikulu jijini Nairobi.
Inaarifiwa huenda Rais Kenyatta akatumia kongamano la wajumbe kutangaza kuwa chama cha Jubilee kiko nyuma ya kinara wa ODM Raila Odinga.
Kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa KICC na naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe awali alikuwa amegusia kuwa wataunga mkono Raila.
"Sisi tutafanya kongamano letu kule KICC nao kina Junet (ODM) watafanya Bomas na kisha sote tutakutana na kutangaza mgombea tunayemuunga mkono," alisema Murathe
Imekuwa wazi kufikia sasa kuwa Rais Kenyatta anamuunga mkono Raila Odinga kama mrithi wake kwenye uchaguzi wa Agosti
Tayari juhudi za kukifufua chama cha Jubilee tangu naibu rais William Ruto na wandani wake wahame zimeanza.
Chama hicho kwa sasa kina nembo na rangi mpya baada ya kuondoa zile zilizokuwa zikihusishwa na DP Ruto.
Kinara wa ODM Raila Odinga amekuwa akiweka wazi kuwa Azimio la Umoja ni muungano wa Jubilee na ODM.
Sisi kama wanaODM na wana Azimio la Umoja, Azimio inaunganisha ODM na Jubilee. Huu ni mwamko mpya, ile Tsunami nilikuwa nikisema kuhusu. Itachukua takataka yote ya Tangatanga na kupeleka baharini," alisema Raila awali

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii