Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.
Akizungumza Leo Jumapili Februari 6,2022 mara baada ya kuchukua fomu hiyo,Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM,Nyongo amesema ameamua kuchukua fomu hiyo kutokana na uzoefu alionao katika uongozi.
Amesema uzoefu alionao ni pamoja na kuwa Naibu Waziri pamoja na kuongoza kamati mbalimbali.
Nyongo ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Bunge ya Maendeleo ya Jamii,amesema anazijua sheria vizuri hivyo anauhakika atamsaidia Spika vizuri kuongoza Bunge.