Ndege kubwa iliyobeba watalii inatua katika uwanja wa Mtemere ulioko ndani ya Hifadhi ya Nyerere, ikitokea Zanzibar.
Wameshuka
watalii wapatao hamsini majira ya asubuhi,Baadae ndege nyingine tatu au
Zaidi hutua tena ndani ya hifadhi hiyo zikitokea visiwani, kuwaleta
wageni wengine kwa ajili ya utalii wa kujionea wanyamapori.
Ndege
hizo kwa idadi tofauti, hushuka katika hifadhi hiyo mpya na kubwa zaidi
nchini mara mbili au tatu kwa wiki, kutoka visiwani.
Idadi ya ndege na watalii hutegemeana na msimu pamoja na idadi ya wageni husika.
Imebainika
kuwa kuna upacha wa ajabu kati ya Hifadhi Mpya ya Nyerere na visiwa vya
Zanzibar, kiasi kwamba ndani ya siku moja watalii hutembelea maeneo
yote mawili kwa wakati mmoja.
Wageni kutoka Urusi, Poland na nchi
zingine za Ulaya ambao hupendelea kufanya utalii wa fukwe, katika
visiwa vya Zanzibar, wamegundua kuwa wanaweza pia kutumia siku moja
ndani ya hifadhi ya Nyerere, kabla ya kurudi tena Unguja,” anaelezea
Seth Mihayo, afisa mhifadhi anayeshughulikia masuala ya Utalii katika
hifadhi mpya ya Nyerere.
Afisa mhifadhi anayeshughulikia utalii katika hifadhi ya Nyerere Seth Mihayo akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa ni rahisi sana watalii kutoka Zanzibar kuja kutalii Nyerere kwakuwa mwendo ni dakika 40 tu.
Kwa mujibu wa mhifadhi Mihayo, ni
rahisi sana kwa watalii walioko Zanzibar kufika Nyerere kuliko wao
kwenda hifadhi nyingine yeyote nchini, kwani ni mwendo wa dakika 40 tu.
“Na
hapa Nyerere, kutokana na uwingi wa wanyamapori, watalii huweza kuona
aina zote za wanyama ndani ya muda mfupi sana, na katika sehemu ndogo
tu, ingawa eneo la hifadhi yenyewe ni kubwa sana,” aliongeza Seth.
Hifadhi ya Nyerere in viwanja sita vya ndege maalum kwa ajili ya kushusha watalii.
Ingawa
ilianzishwa miaka mitatu tu iliyopita, baada ya kumegwa kutoka pori kuu
la akiba la Selous, Hifadhi ya Nyerere bado imeweza kuvutia watalii wa
kigeni Zaidi ya Laki moja kwa mwaka.
Wakala wa Utalii aliyeko
Zanzibar, ambaye ni Raia wa Poland, Tomasz Dworczyk anaeleza kuwa kuna
muamko mkubwa wa wakazi wa nchini Polanda kutaka kuja kutalii Tanzania.
“Awali
walianza na visiwa vya Unguja na Pemba kwa ajili ya utalii wa bahari na
fukwe lakini sasa wamegundua kuwa wanaweza pia kufanya utalii wa
wanyamapori bara, hususan katika hifadhi ya Nyerere ndani ya siku moja
au masaa machache kisha kurejea tena Zanzibar!” alisema Dworczyk.