Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
wamempitisha Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu kuwa mgombea wa nafasi
ya Naibu Spika wa Bunge, jijini Dodoma, Jumanne Februari 8, 2022.
Zungu
amepitishwa na wabunge wote wa CCM baada ya Kamati Kuu ya chama hicho
kupitisha jina lake pekee kati ya wabunge 11 wa chama hicho waliokuwa
wakiomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.