Onyo yatolewa kuhusu matumizi ya muda mrefu ya Paracetamol kwa walio na shinikizo la damu

Watu walio na shinikizo la juu la damu wanaotumia paracetamol kwenye maagizo wanaweza kuongeza hatari ya mshtuko wa moyo na kiharusi, utafiti unapendekeza.


Madaktari wanapaswa kufikiria juu ya hatari na faida kwa wagonjwa wanaoichukua kwa miezi mingi, watafiti wa Chuo Kikuu cha Edinburgh wanasema.

Kunywa dawa za kupunguza maumivu ya kichwa na homa ni salama, wanasisitiza.

Wataalamu wengine wanasema utafiti kwa watu wengi zaidi kwa muda mrefu unahitajika ili kuthibitisha matokeo.

Paracetamol hutumiwa sana duniani kote kama tiba ya muda mfupi ya maumivu ya kichwa na mengineo lakini pia huagizwa wagonjwa kudhibiti maumivu ya muda mrefu, licha ya ushahidi mdogo wa manufaa yake kwa matumizi ya muda mrefu.

Watu nusu milioni - mmoja kati ya kila 10 - huko Scotland walipewa dawa ya kutuliza maumivu mwaka wa 2018. Shinikizo la damu huathiri mtu mmoja kati ya kila watu watatu nchini Uingereza.

Utafiti huo ulifuatilia watu 110 wa kujitolea, thuluthi mbili kati yao walikuwa wakitumia dawa za shinikizo la damu, au shinikizo la damu.

Katika jaribio, waliulizwa kuchukua 1g ya paracetamol mara nne kwa siku kwa wiki mbili - kipimo cha kawaida kwa wagonjwa wenye maumivu makali - na kisha vidonge vya dummy, au placebo, kwa wiki nyingine mbili

Jaribio lilionyesha paracetamol iliongeza shinikizo la damu, "mojawapo ya sababu muhimu zaidi za mshtuko wa moyo na kiharusi" zaidi ya placebo yaani matibabu ya kutuliza akili, daktari wa dawa wa Edinburgh Prof James Dear alisema.

Watafiti hao wanashauri madaktari kuwaanzishia wagonjwa wenye maumivu ya muda mrefu kwa kipimo cha chini cha paracetamol iwezekanavyo na kuwaangalia kwa karibu wale walio na shinikizo la damu na walio katika hatari ya ugonjwa wa moyo.

Mpelelezi mkuu Dk Iain MacIntyre, mshauri wa pharmacology ya kimatibabu, katika NHS Lothian, alisema: "Hii sio kuhusu matumizi ya muda mfupi ya paracetamol kwa maumivu ya kichwa au homa, ambayo ni, bila shaka, ni sawa."

usichokifahamu

Dk Dipender Gill, mhadhiri wa kimatibabu wa dawa na tiba katika Chuo Kikuu cha St George's, London, alisema utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Circulation, umebaini "ongezeko dogo lakini la maana la shinikizo la damu kwa watu weupe wa Uskoti" lakini kuna mengi ambayo bado hayajulikani.

Kwanza, haijulikani kama ongezeko lililoonekana la shinikizo la damu linaweza kudumu kwa matumizi ya muda mrefu ya paracetamol," alisema.

"Pili, haijulikani kwa hakika ikiwa ongezeko lolote la shinikizo la damu linalotokana na matumizi ya paracetamol linaweza kusababisha hatari kubwa ya ugonjwa wa moyo na mishipa."

Utafiti mkubwa wa Marekani hapo awali uligundua uhusiano kati ya matumizi ya muda mrefu ya paracetamol na kuongezeka kwa hatari ya mshtuko wa moyo - lakini haikuweza kuthibitisha moja ilisababisha nyingine.

Na tafiti nyingine ndogo hazijaweza kuthibitisha uhusiano wowote.

Timu ya Edinburgh ilisema hawakuweza kueleza jinsi paracetamol inaweza kuongeza shinikizo la damu lakini matokeo yao yanapaswa kusababisha mapitio ya maagizo ya muda mrefu ya paracetamol.

Hapo awali, dawa hizi zilionekana kuwa salama zaidi kuliko dawa mbadala zenye kupunguza maumivu kama vile ibuprofen, ambazo hufikiriwa kuongeza shinikizo la damu kwa baadhi ya watu.

Shirika la British Heart Foundation, ambalo lilifadhili utafiti huo, lilisema madaktari na wagonjwa wanapaswa kufikiria upya mara kwa mara ikiwa dawa yoyote, hata kitu "kisicho na madhara kama paracetamol," kilihitajika.

Dk Richard Francis, kutoka Chama cha Kiharusi, alisema utafiti zaidi kwa watu walio na shinikizo la damu la kawaida, kwa muda mrefu zaidi, ulihitajika "kuthibitisha hatari na faida za kutumia paracetamol kwa upana zaidi

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii