SERIKALI
kwa kushirikiana na kampuni ya CRRC International ya China wamesaini
mkataba wa ununuzi wa mabehewa 1,430 ya mizigo ya Reli ya kisasa- SGR
mkataba huo utakaogharimu Dola za kimarekani milioni 127.2.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Masanja Kadogosa, amesema mkataba huu ni wa miezi kumi na mbili na
utahusisha usanifu na utengenezaji wa Mabehewa kwa ajili ya kubeba
mizigo ya aina mbalimbali kulingana na aina ya behewa na matakwa ya
mteja kupitia reli ya kisasa.
Aidha Kadogosa alisema ujio wa
mabehewa hayo yatasaidia kusafirisha vitu mbalimbali kama Mifugo,
Sukari, Chumvi, Pamba, Tumbaku, Kahawa na magari ambayo kwa kiasi
kikubwa yanasaidia kukuza biashara ndani na nje ya nchi kama Uganda.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC) Masanja
Kadogosa amesema mkataba huu ni wa miezi kumi na mbili na utahusisha
usanifu na utengenezaji wa Mabehewa kwa ajili ya kubeba mizigo ya aina
mbalimbali kulingana na aina ya behewa na matakwa ya mteja kupitia reli
ya kisasa.
Aidha Kadogosa alisema ujio wa mabehewa haya
yatasaidia kusafirisha vitu mbalimbali kama mifugo,sukari, chumvi,
pamba, tumbako, Kahawa na magari ambazo kwa kiasi kikubwa zitasaidia
kukuza biashara ndani na nje ya nchi kama Uganda, Rwanda, Burundi na
congo kwa kurahisisha usafirishaji na kupunguza gharama za matengenezo
ya barabara.
Pia Kadogosa alisema faida za mabehewa hayo ni
kwamba yataraisisha biashara ya usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya
kisasa kwa umbali wa km 500, hivyo unatarajia kukamilika kwa manunuzi na
kuwasili kwa mabehewa hayo February 2023.
Akizungumza
katika Hafla hiyo leo jijini Dar es salaam Waziri wa ujenzi na Uchukuzi
Prof. Makame mbarawa Serikali imedhamiria kuhakikisha huduma ya usafiri
wa mizigo inaimarika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kwa lengo la
kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi.
‘Ujenzi wa Reli ya
kisasa unaoendelea hivi sasa kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro
ambacho kimefika 95%, Morogoro – Makutupora ambacho kimefika 81% na
kipande cha Mwanza – Isaka ambacho kimefika 4% ni ishara tosha kwamba
Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu
Hassan imedhamiria kuongeza ufanisi na kuboresha huduma ya usafiri na
usafirishaji kupitia reli’amesema Waziri Prof Mbarawa.
Aidha,Profesa
Mbarawa amesema kutokana na uwezo mkubwa wa reli ya kisasa Behewa hizo
zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mrundikano wa mizigo katika
bandari ya Dar es Salaam ambapo treni moja itakuwa na uwezo wa kubeba
Tani 10,000 kwa mkupuo ambayo ni sawa na malori 500.