Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 09 Februari, 2022. amemuapisha Dkt. Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Kiapo hicho kimefanyika mbele ya Makamu wa Arais Dkt. Philip Isdory Mpango, Waziri mkuu Kasiim Majaliwa, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, na Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhwan Kikwete