Abiria mmoja alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow baada ya mwanamke mmoja kusema alibakwa kwenye ndege wakati wa safari ya usiku ya kuvuka Atlantiki kutoka New Jersey.
Mwanamke huyo alisema alishambuliwa na mwanaume mwenye umri wa miaka 40 huku wengine wakiwa wamelala kwenye ndege kutoka Newark tarehe 31 Januari.
Maafisa walipanda ndege ya United Airlines baada ya kutua saa 06:39 GMT na kumkamata mtu huyo ambaye ameachiliwa huru kwa ajili ya uchunguzi.
Polisi wa Met walisema mwanamke huyo alikuwa akiungwa mkono na maafisa maalum.Msemaji alisema Met wanafahamu kuhusu "tukio la ndege inayoingia"