Ibada ya Kumbukizi miaka 5 kifo cha Mkapa kufanyika Masasi

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo wastaafu, pamoja na wananchi wa Kata ya Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara wamejitokeza kwenye Ibada maalum ya kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha Hayati Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu Awamu ya Tatu huku mgeni rasmi wa Kiserikali akiwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.

Ambapo Dk Hussein Mwinyi, leo Julai 23, mwaka huu amewasili katika  Uwanja wa Ndege wa Nachingwea, Mkoa wa Lindi tayari kuelekea Lupaso, Mtwara, kuhudhuria ibada maalumu ya kumbukumbu ya miaka mitano ya kifo cha Rais wa awamu ya tatu, hayati Benjamin Mkapa.

Alipowasili alipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, pamoja na  viongozi mbalimbali wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Mkapa alifariki dunia Julai 24, 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi. 

Mkapa alifariki dunia akiwa na miaka 81 na ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu alipozindua kitabu cha maisha binafsi ya Rais mstaafu wa Tanzania, kinachoitwa ‘My life, My purpose’ (Maisha Yangu, Kusudio Langu).


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii