Ujerumani imewarudisha kwao raia 43 wa Iraq julai 22 mwaka huu wakisafirishwa kwa ndege ya kukodi iliyokuwa ikielekea Baghdad
Ndege hiyo ikiwa na Wairaqi 43 imliondoka, siku chache baada ya ndege kama hiyo kuwarudisha nyumbani raia wa Afghanistani. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Ndani Alexander Dobrindt anajadili mbinu kali zaidi za uhamiaji nchini Denmark.
Wizara ya Sheria ya jimbo la mashariki la Thuringia imesema wote waliorudishwa kwao walikuwa "wanaume," waliotakiwa kuondoka nchini, na kuongeza kuwa baadhi yao "waliwahi kuhukumiwa kwa makosa ya jinai siku za nyuma."
Wakati huo huo, mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wanakutana katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen, tangu siku ya Jumanne kwa mazungumzo kuhusu namna bora ya kukabiliana na wahamiaji haramu na uhalifu uliopangwa.
Miongoni mwao ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Alexander Dobrindt, ambaye wiki iliyopita alipendekeza sera kali ya uhamiaji ya Ulaya katika mazungumzo na wenzao kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwarejesha makwao waomba hifadhi waliokataliwa katika nchi kama vile Syria na Afghanistani.