Wavuvi mkoani Geita waongezewa mitaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan omeongeza mara 50 mitaji ya wavuvi mkoani Geita ikiwa ni ongezeko jipya la Shilingi milioni 770.

Rais Samia katika kuendelea kuimarisha sekta ya uvuvi nchini, ameongeza mitaji kwa wafugaji wa samaki mkoani Geita kutoka Shilingi 14, 000, 000 mwaka 2021 hadi Shilingi 792,563,616.24 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la Shilingi 778,563,616 sawa na 57%, hii imechechemua uchumi wa

Geita na kuchochea maendeleo katika sekta ya uvuvi, lakini pia, idadi ya vizimba vya kufugia Samaki imeongezeka kutoka 4 mwaka 2021 hadi vizimba 27 mwaka 2025 ikiwa na sawa na ujenzi wa vizimba vipya 23 ndani ya miaka minne (4).


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii