MV Tennesee yateketea kwa moto wawili wafariki Kigoma

Watu wawili wamefariki dunia baada ya meli ya MV Tennesee kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kushika moto usiku wa kuamkia leo katika Bandari ya Kigoma, karibu na kituo kikuu cha Reli. 

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kigoma, Mrakibu Msaidizi Michael Maganga, ajali hiyo imesababisha uharibifu wa mali, ingawa thamani halisi ya hasara bado haijajulikana. 

Kamanda Maganga amesema kuwa uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo halisi cha moto huo. 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii