Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ametangaza kuwa Ufaransa itatambua rasmi Taifa la Palestina mwezi Septemba mwaka huu, katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani imesema kuwa uamuzi huo utaifanya Ufaransa kuwa nchi ya kwanza ndani ya kundi la mataifa tajiri ya G7 kuchukua hatua hiyo.
Kupitia chapisho kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), Macron amesema: "Lenye uhitaji mkubwa hii leo ni kukomeshwa kwa vita huko Gaza na raia waokolewe. Amani inawezekana kufikiwa. Tunahitaji usitishaji mapigano mara moja, kuachiliwa kwa mateka wote, na msaada mkubwa wa kibinadamu kwa watu wa Gaza."
Macron ameongeza kuwa uamuzi huo ni sehemu ya msimamo wa Ufaransa wa muda mrefu kuhusu haki ya Wapalestina kuwa na taifa lao, sambamba na kuhakikisha usalama wa Israel na kuondolewa kwa kundi la Hamas.
Katika chapisho lake, amrsema: “Mkweli kwa ahadi yetu ya kihistoria kwa haki na amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati, nimeamua kuwa Ufaransa itatambua Jimbo la Palestina.”
Akiambatanisha barua rasmi kwa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas, Macron amesisitiza kuwa ujenzi wa taifa la Palestina unapaswa kwenda sambamba na kuondoa vikosi vya Hamas, kulinda Gaza, na kuhakikisha usalama kwa pande zote katika Mashariki ya Kati.