Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa kesho Julai 26 mwaka huu kutakuwa na Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa na utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu Halmashauri Kuu Taifa utakaoendeshwa kwa njia ya mtandao.
Akitangaza mkutano huo, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla amesema, agenda kuu ya Mkutano huo Mkuu Maalum ni marekebisho madogo ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi.
Aidha Mhe. CPA Makalla amethibitisha jambo hilo kutokana na uvumi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa mkutano huo huku akiendelea kubainisha kuwa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika katika wilaya na mikoa yote.