Kuwashwa kwa mwenge wa mashujaa

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri amesema tukio la uwashaji mwenge wa mashujaa katika maadhimishio ya Siku ya Mashujaa waliopigania Uhuru na kulinda mipaka ya nchi ni ishara ya kuimarisha uzalendo, heshma na kuwaelimisha vijana kuhusu historia ya taifa la Tanzania.

Shekimweri amesema hayo jijini Dodoma wakati akiwasha mwenge wa mashujaa ambapo ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi wakati wa maombolezo ya mashujaa hao ambayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Julai 25 mwaka huu.

Aidha amewataka watanzania kutumia madhimisho hayo kulinda amani iliyopo nchini hususani katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mwenge wa mashujaa umewashwa majira ya saa sita usiku katika viwanja vya Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii