Msanii wa kizazi kipya Kevin Peter Stanley maarufu kama Kevin Cash ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la #teketeza akiwa amemshirikisha Jaiva
Wimbo huo wenye maadhi ya Amapino umetayarishwa na Kapipo huku mtayarishaji mkubwa wa Muziki Nchini Tanzania Lizer Classic akihusika kuchanganya na kuweka ustadi wa sauti kwenye wimbo huo
Teketeza inakuja wakati huu ambao Kevin Cash anaendelea kutamba na wimbo wake wa Fire Burning wenye maadhi ya R&B na Afrobeat ukiwa na zaidi ya watazamaji 25,000 kwenye mtandao wa YouTube
Tangu kuingia rasmi kwenye Muziki mwaka 2024 , Kevin Cash amefanikiwa kuachia nyimbo sita mpaka sasa ambazo ni Lolo,Pesa,Koko,Khululek,Fire burning na Teketeza huku pia akifanikiwa kupata collabo na Wasanii wakubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Umahili wake kwenye kufanya aina mbalimbali za Muziki umemfanya Kevin Cash kuwa kipenzi cha Vijana wengi ambao ni mashabiki wa Muziki, hili linathibitishwa na mapokezi makubwa yaliyopo kwenye kazi zake sambamba na mapokezi anayoyapata kwenye majukwaa mbalimbali ya Muziki kama Chuo Kwa Chuo Tamasha linaloandaliwa na Msanii Billnass
Kwa sasa Audio ya wimbo huo inapatikana katika majukwa yote yanayotumika kusikiliza Muziki, ikiwa ni pamoja na YouTube, Audiomark,Spotify, na Boomplay.