Msanii na Mtayarishaji
wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania (Bongo Fleva), Mocco Genius
amewauliza wadau na mashabiki wa muziki huo kuwa watampatia “Ufalme” wake kwa
hiari, au auchukue kwa lazima?
Kupitia ukurasa wake wa
Instagram, Mocco Genius amesema kuwa yeye ndiye aliyetambulisha style ya Kompa
nchini hasa kupitia nyimba mbali mbali kama vile MI NAWE (Feat. Marioo),
MCHUCHU (Feat. Ali Kiba), FITINGI (Feat. Marioo) na nyinginezo kadhaa, sasa
hivi wasanii wengi wanaufanya.
Hivyo akaamua kuhoji
kama wadau wako tayari kumpatia Ufalme wake au auchukue kwa Lazima.
Wewe unashauri nini?