Mwanamke mmoja nchini
Marekani ameamua kufungua mashitaka dhidi ya wanandoa wawili na waandaaji wa
harusi aliyohudhuria kuwa kutokuifurahia harusi hiyo na utaratibu wote
kiujumla.
Kupitia mtandao wa
REDDIT, mwanamke huyo ambaye hakujitambulisha jina lake amesema kuwa amefikia
hatua hiyo baada ya kutokuifurahia sherehe hiyo iliyokuwa imejawa na mapungufu
mengi tofauti na vile ambavyo ilitarajiwa hasa kupitia kile kilichokuwa
kimeainishwa katika taarifa za mwaliko
Katika maelezo yake ni
kwamba, Sherehe hiyo ilifanyika katika eneo la uwazi yaani “outdoor” tofauti na
ilivyoelezwa katika mwaliko, na kulikuwa na hali ya joto kali kutokana na jua
kali. Pia ameongeza kuwa kelele za watoto wadogo takribani 8 zilikuwa ni kero
kubwa sana wakati wa shughuli hiyo huku wazazi na waandaaji wakishindwa kuchukua
hatua yoyote na kusababisa usumbufu kwake na waalikwa wengine
Mwanamke huyo hakuishia
hapo, pia amelalamikia kitendo cha Bibi harusi na kaka yake kuanzisha vurugu za
mara kwa mara kwa bwana harusi, hali ambayo ilifanya ratiba kusimama mara kwa
mara na kusababisha usumbufu mkubwa.
Aidha kilichomkera
zaidi, ni chakula cha waalikwa kuwa na wadudu aina ya Inzi hali iliyomfanya
asifurahie chakula hicho na kupelekea kupata matatizo ya Tumbo. Na katika
kuongezea juu ya hilo, Bibie huyo anadai kuwa alitozwa kiasi cha USD 2 (Tshs
5,130) pale alipoenda upande wa Bar ilyokuwepo eneo ili kujipatia maji ya
kunywa kutokana na joto kuwa kali sana