Salim Kikeke miongoni mwa wagombea ubunge Jimbo la Moshi Vijijini.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo Julai 29 mwaka huu katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu jijini Dodoma imeelezwa kuwa wagombea saba wamepitishwa katika hatua ya awali ya kugombea ubunge wa Jimbo la Moshi Vijijini.

Miongoni mwa waliopitishwa ni mwanahabari na mtangazaji maarufu, Salim Kikeke, ambaye jina lake limeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ushawishi wake wa muda mrefu katika tasnia ya habari.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii