Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amewataja Funti Majala, Amina Bakari, Hamis Mkotya, Juma Nkamia, Omary Puto na Francis Julius kuwa ndiyo watiania wa ubunge wa Chemba waliopendekezwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwenda hatua ya kupigiwa kura za maoni.
Ukiacha jimbo hilo, amesema walioteuliwa katika Jimbo la Kondoa Mjini ni Ally Makoa, Mariam Mzuzuri, Ally Juma na Dk Athuman Nchana.
Makalla ameyasema hayo leo, Jumanne Julai 29, 2025 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Amesema watiania watano wameteuliwa katika Jimbo la Kondoa Vijijini, ambao ni Ashatu Kijaji, Said Mnyeke, Hassan Lubuga, Juma Shaaban na Hans Kida.
Katika Jimbo la Mpwapwa, Makalla amesema watiania saba wameteuliwa ambao ni George Malima, Yamasi Chiwanga, Zakayo Mkemwa, Adam Michael Malima, John Fusi, Magreth Lema, Ever Mpagama, huku jimbo la Kibakwe wakiteuliwa watano ambao ni George Simbachawene, George Kahela, Dk Kwame Mwaga, Nelson Nyami na Amani Bendera.
Katika Jimbo la Dodoma Mjini, wanane wameteuliwa ambao ni Rashid Mashaka, Pascal Chinyere, Samwel Malecela, Samwel Kisaro, Fatma Waziri, Robert Minje, Rosemary Nyairo na Abdallah Manyemba.
Wakati huohuo, katika Jimbo la Mtumba watiania wanne wameteuliwa ambao ni Anthony Mavunde, Mussa Muhamo, Anthony Kanyama na Juma Karabaki.