SAKATA la
Rapa Jay Z na Kijana anayedai kuwa ni Mtoto wake halali hatimaye limefikia
ukumbini baada ya Kijana huyo kuiomba mahakama kufutilia mbali mashitaka hayo.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram, Kijana Rymir Satterthwaite (30) alichapisha kipande
cha video kikimuonesha kuthibitisha kuwa ameamua kuachana na Kesi aliyoifungua
dhidi ya Jay Z kuwa ni baba yake mzazi na amemtelekeza kwa kipindi cha muda
mrefu tangu alipomuacha mama yake akiwa mjamzito.
Rymir
ameongeza kuwa, kuachana na kesi hiyo sio kwamba ameshindwa kuendelea nayo,
bali ni maamuzi yake na utashi wake binafsi ambavyo vimemsukuma kufikia hatua
hiyo, ili aweze kuendelea na maisha mengine kama ambavyo ilikuwa hapo awali.
Ikumbukwe
kuwa, Kijana huyo ilijitokeza miaka kadhaa iliyopita akisema kuwa yeye ni mtoto
halali wa Jay Z ambaye alikuwa na mahusiano na mama yake (Rymir) miaka ya 1990 ,
hivyo anahitaji haki yake ya msingi kimalezi kutoka kwa baba yake.
Hata hivyo,
Jay Z alijitokeza hadharani na kukana kauli ya kijana huyo, huku akiitaka
mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo, kwa sababu hata vipimo vya DNA
havikuthibitisha kama Rymir ni mtoto wake kibaiolojia.