MSANII wa
Muziki wa Popnchini Marekani, Katty Perry, hatimaye “amezama” katika penzi
jipya na Waziri Mkuu mstaafu wa Canada, Justin Trudeau zikiwa zimepita wiki
chache tangu ithibitishwe kuwa ameachana
na aliyekuwa mchumba wake Orlando Bloom.
Perry (40) na Trudeau (50) walinaswa na Kamera za mmoja wa mashabiki wa muziki wake katika mgahawa maarufu nchini Canada, unafahamika kwa jina la Le Violon, na wawili hao walikuwa katika mazungumzo yenye furaha nzito huku yakitawaliwa na chembechembe za mahaba mazito ndani yake.
Ingawa
wawili hao hawajathibitisha rasmi kuhusu uhusiano huo, lakini viashiria vyote
vilivyoonekana katika Mgahawa huo, vilijenga taswira ya kuwepo kwa mahusiano
baina ya wawili hao.
Trudeau
aliachana na Mke wake Sophie Gregoire Trudeau mwaka 2023 baada ya kudumu katika
ndoa kwa muda wa miaka 18 wakifanikiwa kupata watoto watatu, na mnamo mwezi
Januari mwaka huu, aliamua kujiuzuru nafasi ya Waziri Mkuu nchini Canada
kutokana na masuala mbali mbali ya kiuongozi.
Kwa Upande
wa Katty Perry yeye amefanikiwa kupata mtoto mmoja na aliyekuwa Mchumba wake,
Orlando Bloom