MSANII wa
muziki wa Bongo Fleva, Baba Levo ametoa ombi lake kubwa kwa wasanii mbali mbali
hapa nchini baada ya jina lake kupitishwa kati ya wagombea Sita watakaopitia mchujo wa pili wa
kuipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye nafasi ya Ubunge
Kigoma Mjini.
Katika
Melezo yake, Baba Levo amewaomba wasanii hao ambao wanamuunga mkono kwa moyo
mmoja, kurekodi vipande vya Video wakimuombea Kura kwa wajumbe ambao ndio wana
jukumu la kukamilisha mchakato unaofuata.
Baba Levo
alitajwa kuwa miongoni mwa watia nia wengine (6 Bora) ambao sasa Wajumbe ndo
watakaoamua nani mwenye sifa za kupiga hatua Zaidi.