Ifikapo 2050 uchumi wa kila Mtanzania kwa siku ni Sh50,000

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Tanzania ina uwezo wa kufikia uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2050, ikiwa wananchi wataongeza bidii na tija katika kazi.

Akizungumza katika uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma, Profesa Kitila amesema malengo yaliyowekwa kwenye dira hiyo ni kufikisha pato la mtu mmoja mmoja kufikia Dola za Kimarekani 7,000 kwa mwaka, sawa na wastani wa Sh50,000 kwa siku.

“Kwa hali yetu ya uchumi ikifika mwaka 2050, tukifanya bidii kubwa, tuna uwezo wa kufika uchumi wenye thamani ya Dola za Kimarekani 7,000 kwa mtu kwa mwaka. Ni sawasawa na Sh50,000 kwa siku,” amesema Profesa Kitila.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii