Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema zipo shabaha 18 za Dira ya Taifa ya mwaka 20250 ikiwemo Tanzania kuwa Mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika na miongoni mwa nchi kumi bora duniani lakini pia Mtanzania kuishi wastani wa miaka 75 yenye afya na furaha.
“Shabaha nyingine ni Tanzania kuwa Mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika na miongoni mwa nchi kumi bora duniani, Mtanzania kuishi wastani wa miaka 75 yenye afya na furaha, Watoto wote wa kike na wa kiume wana fursa sawa ya malezi bora ya utotoni, huku angalau asilimia 90 ya watoto wote wakiwa katika hatua sahihi za ukuaji unaoonesha uwezo wao kamili ifikapo umri wa miaka mitano”
“Kutokomeza vifo vya wajawazito, watoto wachanga na Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, huduma bora za afya kwa wote, mfumo bora na jumuishi wa elimu na mafunzo katika ngazi zote, Watoto wote wa kike na wa kiume wana fursa sawa za kupata elimu ya awali yenye kujenga msingi imara kwa ajili ya kujifunza na kujielimisha bila ukomo”
“”Watanzania wote wanapata elimumsingi bora (miaka sita ya elimu ya msingi na miaka minne ya sekondari) na angalau asilimia 25 wanapata elimu ya juu, upatikanaji wa huduma jumuishi za hifadhi ya jamii kwa wote, upatikanaji sawia wa maji safi na salama, huduma za usafi wa mazingira, na nishati safi, angalau asilimia 50 ya Watanzania wana ajira zenye staha katika
sekta rasmi”
“Kuwa na viwango vya juu vya uhifadhi wa mazingira na uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi na kuifanya Tanzania kuwa kati ya nchi kumi bora barani Afrika, Jamii yenye umahiri wa kidijitali, ambapo asilimia 70 ya wananchi wanakuwa na ujuzi wa TEHAMA, zaidi ya asilimia 80 ya huduma za serikali zinatolewa kwa njia ya kidijitali, na hivyo kuwezesha wananchi wote kupata huduma za msingi kwa urahisi”
“Kuongezeka kwa matumizi ya nishati ya umeme kufikia wastani kwa 3,000 Kwh kwa kila mtu kwa mwaka, Tanzania kuwa kinara barani Afrika na miongoni mwa nchi kumi bora duniani katika kupunguza pengo la kijinsia kwa angalau asilimia 85”