Watafiti kutoka chuo
kikuu cha Flinders kilichopo nchini Australia, wamesema kuwa mawasiliano ya
ishara kwa njia ya jicho, ndiyo njia sahihi Zaidi inayoweza kukupatia kile
unachohitaji ndani ya muda huo kwa haraka Zaidi.
Inafahamika kuwa mara
nyingi Jicho/Macho hutumika kuwasiliana kwa njia ya siri kati ya watu wawili au
Zaidi, lakini ndiyo lugha ya ishara ambayo mara nyingi urahisi wake katika
kufikisha ujumbe huwa ni mkubwa Zaidi ndani ya muda mfupi
Dr. Nathan Caruana
ambaye ni Mkufunzi na Mtafiti katika chuo hicho, amesema kuwa wamefanikiwa
kufanya utafiti kwa watu Zaidi ya 137 kwa kuwahoji maswali mbali mbali kwa
nadharia na vitendo, kisha kubaini kuwa siri kubwa iliyojificha katika ishara
kwa njia ya jicho/macho ni kwamba inarahisisha zaidi mawasiliano.
Aidha Dr. Caruoana
ameongeza kuwa, iwapo itatokea mtu akahitaji msaada wa kitu flani ambacho kipo
mbali na anahitaji aliye karibu nacho ampatie, basi akimtizama na kukitizama
kitu hicho kwa wakati mmoja, ni rahisi sana kukipata tofauti na vinginevyo.
“Hata ikatokea una
hisia na mtu, ukimkonyeza tu ataelewa hitaji lako. Achilia mbali suala hilo,
umakini wa kumtazama mtu wakati anaongea, huashiria anachokisema unakielewa.
Pia kama mtu amekosea, unaweza kumwambia kwa siri kupitia jicho lako na
akajirekebisha” alisema Mtafiti huyo