Msanii wa bongo fleva barani Afrika, Diamond Platnumz ametamba kununua miwani ya bei mbali ya zaidi ya shilingi milioni 8 za Kitanzania kutoka kwa dizaina maarufu duniani.
Diamond ametoboa siri hiyo baada ya kuachia vipande vya video vikimuonesha akinunua miwani kwenye duka la bling’ibling’I huko nchini Marekani.
Pia ameonesha risti aliyonunulia miwani hiyo ikionesha wazi kuwa amenunua pea tisa za miwani.
Miwani hiyo inaonesha nembo za kampuni kubwa za urembo duniani za Dolce & Gabbana, Gucci, Dior na Prada.
Miwani hiyo imemgarimu Diamond Dola za Kimarekani 3,510 (zaidi ya shilingi milioni 8,073,000 za Kitanzania.