Waziri wa Elimu afutwa kazi kwa tuhuma za utovu wa nidhamu

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amemvua wadhifa wake Waziri wa Elimu ya Juu, Nobuhle Nkabane, kufuatia tuhuma nzito za utovu wa nidhamu na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Ikulu ya Afrika Kusini, Nkabane anatuhumiwa kwa kutumia nafasi yake kuwateua watu wa karibu na chama chake cha ANC kushika nyadhifa katika bodi za mashirika ya kukuza ujuzi, kinyume na taratibu za kiutumishi. Aidha, inadaiwa alitoa taarifa za uongo bungeni ili kuficha vitendo hivyo.

Rais Ramaphosa amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa kwa lengo la kuimarisha misingi ya uwajibikaji serikalini na kurejesha imani ya wananchi kwa uongozi wa nchi. Taasisi za kisheria na maadili zimetaarifiwa kuendelea na uchunguzi wa kina kuhusu madai hayo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii