Waumini wa Gwajima waendelea na kesi mahakamani leo

Kesi ya Kikatiba nambari 16408 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa na Dinali Mbaga na wenzake 51 ambao ni waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima (Glory Of Christ Tanzania Church) inaanza kusikilizwa leo Julai 22, 2025 kwa ajili ya mahakama kupanga utaratibu wa shauri hilo na kutoa uelekeo.

Waumini hao 52 wanadai kufanyiwa vitendo visivyo sawa kisheria ikiwemo kupigwa juni 29, 2025 wakati wakifanya ibada.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, ambapo waumini hao waliwasilisha shauri hilo Mahakamani chini ya hati ya dharura iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala wakiieleza Mahakama kuwa udharura wa kesi unatokana na shauri hili linagusa haki nyeti sana ya Uhuru wa Dini, na wa kuabudu.

Kesi hiyo itasikilizwa kwa njia ya mtandao chini ya Jopo la Majaji Watatu, ambao ni Mkeha, Maruma na Kisanya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii