Biashara 15 zapigwa marufuku kufanywa na wageni

SERIKALI imetoa amri ya katazo la wasio raia wa Tanzania kufanya biashara za aina 15 smri hiyo imechapishwa Julai 28, mwaka huu katika Gazeti la Serikali namba 487A iliyotolewa chini ya Kifungu cha 14A (2) cha Sheria ya Leseni za Biashara (Sura ya 101). 

Shughuli hizo ni pamoja na biashara ya uuzaji wa bidhaa kwa jumla na rejareja bila kujumuisha maduka makubwa, maduka maalumu ya bidhaa na vituo vya jumla kwa wazalishaji wa ndani na uhamisho wa fedha kwa simu. 

Zingine ni ukarabati wa simu za mkononi na vifaa vya kielektroniki, biashara za saluni isipokuwa biashara inayofanywa hotelini au kwa madhumuni ya utalii, usafi wa nyumba, ofisi na mazingira na uchimbaji mdogo. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii