Wimbo Wa Nandy "TONGE NYAMA" Waondolewa Youtube. Mwenyewe Atoa malalamiko


Vizualizer (Video Taswira) ya Wimbo wa “Tonge Nyama” kutoka kwa msanii Nandy akiwa amemshirikisha Marioo, imeondolewa katika mtandao wa Youtube baada ya malalamiko ya Hakimiliki juu ya jina hilo kutoka kwa msanii na muandaa matamasha nchini anayefahamika kwa jina la MR TONGE NYAMA.


Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Nandy amethibitisha hilo huku akitoa malalamiko makubwa na kuhuzunishwa na hatua ya kuuondoa wimbo huo (Video) katika mtandao wa Youtube licha ya kuwa alitoa ufafanuzi juu ya kutumia jina hilo pasipo na nia ya kujinufaisha kibiashara kama mlalamikaji anavyodai.


Aidha Nandy ameongeza kuwa alichokifanya ilikuwa ni Sanaa na amewekeza kwa kiwango kikubwa, hivyo jambo hilo hawezi kukubaliana nalo, na amewaachia wanasheria washughulikie


“BRO NAANDIKA KWA UCHUNGU SANA NALIA KWA HASIRA SANA. NILIKAA KIMYA ILI USHAURIANE NA LAWYER WAKO KAMA MKO SAHIHI SABABU MLINIPA BARUA NIKIWA NIMEWEKA VIDEO TU YA WATOTO WANAKULA MKASEMA NIMETUMIA JINA LAKE KWA FAIDA ZANGU BILA KUJUA NI WIMBO! WIMBO UMETOKA NIKAJUA MTAKAA CHINI MUELEWE KUWA SIKUWA NA NIA YA ILO MNALOSEMA JINA LENU BALI NIME FANYA SANAA KAMA WATU WENGINE KUMBE HAMKUTOSHEKA? KAKA MMENDA KUFUTA WIMBO WANGU YOUTUBE? INVESTMENT YANGU YOTE MNATAKA IZIMA SABABU UNAITWA TONGE NYAMA? MMENIKOSEA NILITEGEMEA WEWE NI KIJANA UNATAFUTA BASI KILA MTU ATAFUTE KWA AMANI ILA HUKUTAKA IVYO UMETAKA NIUMIE NIRUDI NYUMA! HII SIWEZI VUMILIA WE ARE DOING TOO MUCH WE ARE INVESTING TOO MUCH SIJUI KAMA HATA UNAELEWA DAAH! ACHA LAWYERS WETU WAONGEE ILA ASANTE.” Aliandika Nandy


   MALALAMIKO YENYEWE  


Kwa Mujibu wa Barua iliyoandikwa na mwanasheria wa mlalamikaji ambaye ni Mr. Tonge Nyama tarehe 23/7/2025, imeainsha kuwa Nandy kupitia video hiyo, ametumia jina la TONGE NYAMA ambalo mlalamikaji amekuwa akilitumia katika matamasha mbali mbali ya chakula, ikiwemo mashindano ya kula chakula, na wala hakuombwa ridhaa yoyote juu ya matumizi ya jina hilo.


Pia barua hiyo imeainisha kuwa, katika Video hiyo ya “Tonge Nyama” kutoka kwa Nandy, imetumia maudhui ya chakula yanayofanana na maudhui ambayo mlalamikaji huyafanya mara kadhaa katika matamasha yake, kitu ambacho kinaashiria ukiukwaji wa taratibu za hakimiliki kwa makusudi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii