Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Makelele nchini Uganda, Tumwine Elson anatarajia kuhukumiwa hivi karibuni nchini humo baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya Kompyuta na mitandao ya kijamii kinyume na sheria.
Taarifa kutoka nchini Uganda zinadai kuwa, Tumwine ambaye ni mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu chuoni hapo aliripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha mnamo Juni 8, 2025 wilayani Hoima alipokuwa akitekeleza Mafunzo kazini
Kupotea kwake kulizidi kuteka vichwa mbali mbali vya habari kwa takriban mwezi mzima, mpaka ambapo wiki hii ilipobainika kuwa Tumwine alikuwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii nchini humo
Akiwa katika Mahakama ya Entella, mwanafunzi huyo alisomewa mashitaka hayo ambayo hakimu alieleza kuwa, Tumwine alichapisha video ya uchochezi katika ukurasa wake wa Tik-Tok na akiwakashifu na kuwadhalilisha viongozi wa ngazi za juu serikalini, akiwemo Spika wa Bunge la Uganda na Rais wa Uganda Yoweri Mseveni, jambo ambalo ni kinyume na sharia za kimitando na Kompyuta nchini humo
Mahakama ilimkuta Tumwine na Hatia huku mtuhumiwa akiomba msamaha ili arudi uraiani, na kinachosubiriwa hivi sasa ni hukumu dhidi yake.