wanahabari watakiwa kutumia taaluma yao vyema wakati wa kampeni

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele, amewataka wanahabari kote nchini kutumia taaluma yao kwa weledi katika kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu  ili kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwa amani na utulivu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kitaifa kati ya INEC na waandishi wa habari ulioandaliwa kwa lengo la kuwaandaa vyema wanahabari kuelekea uchaguzi huo, Jaji Mwambegele amesema  ni muhimu vyombo vya habari kuwa chanzo cha maarifa sahihi na yenye kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mchakato wa kidemokrasia.

“Tunahitaji wanahabari kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha wananchi juu ya mchakato wa uchaguzi. Habari zenu zinaweza kuwa chachu ya wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Oktoba kwa amani na utulivu,” alisema Jaji Mwambegele.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii