Rapa na Emcee kutoka Uingereza mwenye asili ya Zimbabwe Rhyme Assassin ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Be Might
Kupitia wimbo huo uliotayarishwa na Deep Voice , Rhyme Assassin amewashirikisha Stic Man ( Dead Prez ) pamoja na Wayne Gidden
Be Mighty ni wimbo unao hamasisha watu kutokukata tamaa na kusimama imara katika kila jambo ili kutimiza malengo ama shabaha walizojiwekea
Kabla ya kuja na Be Mighty , Rhyme Assassin aliachia wimbo wa kushirikiana unaoitwa Hit Em Up ukiwa kama wimbo wa pili wa utangulizi kwenye album yake mpya " Rhyme Assassin " inayotarajiwa kutoka mwaka huu 2025
Kupitia wimbo huo Rhyme Assassin aliwashirikisha M.O.P na James Brown kutoka Ruste Juxx, huku kwenye upande wa video ya wimbo huo iliongozwa na Entity Production
Rhyme Assassin ni miongoni mwa Emcee wenye uwezo wa kurap kwenye beat mbalimbali. Neno Rhyme kwenye jina lake ni kielelezo cha ushairi wake lakini neno Assassin kisanaa linaashiria uwezo wake ambao ni kipaji cha juu sambamba na ubunifu