Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha United Democratic Party (UDP), Saum Hussein Rashid, akiambatana na mgombea mwenza wake Juma Khamis Faki, wamechukua fomu za uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Njedengwa jijini Dodoma.
Baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Bi. Saum amesema kipaumbele chake ni kuwainua wananchi wanyonge kiuchumi na kuwaondolea changamoto zinazowakabili.
"Lengo kubwa la chama chetu kuomba ridhaa ya Watanzania ni kuwainua wananchi wanyonge, kama ambavyo sera yetu ya ‘kuwajaza watu mapesa’ tumekuwa tukiiongea muda mrefu," amesisitiza.