Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD) Doyo Hassan Doyo amesema hajawahi kupewa upendeleo wowote kwa sababu ya nafasi yake kisiasa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari Doyo amesisitiza kuwa kwake siasa imekuwa ni uwanja wa kushindana kwa hoja na sera, siyo chanzo cha kupata manufaa binafsi.
“Sijawahi kupata upendeleo eti kwa sababu mimi ni mwanasiasa. Kila kitu nimepata kwa jasho langu na kwa kushirikiana na wananchi,” amesema Doyo.
Aidha amebainisha kuwa tangu alipoingia kwenye siasa hajawahi kuwa na ugomvi au mifarakano na mtu, akisema falsafa yake ni kuunganisha watu na kuleta mshikamano wa kitaifa badala ya migawanyiko.