Mgombea udiwani wa ACT anadaiwa na Salum Mwalimu mkoani Mara

Katika hali isiyotarajiwa na ya kuvutia katika medani ya siasa za upinzani nchini, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Salum Mwalimu, amemnadi hadharani mgombea udiwani wa chama cha ACT-Wazalendo, Charles Machemba katika Kijiji cha Kata ya Ikoma mkoani Mara.

Hatua hiyo imeibua gumzo katika medani ya siasa mjadala mpya kuhusu mshikamano wa vyama vya upinzani na uwezekano wa kuunganisha nguvu katika baadhi ya maeneo ili kuleta mabadiliko halisi kwa wananchi.

Mwalimu licha ya kuwa kwenye kampeni ya kuwania urais kupitia Chaumma mkoani Mara amesisitiza umuhimu wa kuweka kando tofauti za kiitikadi pale panapohitajika uongozi bora.

“Nipo tayari kumpatia ushirikiano hadi atoboe kuwa diwani hapa,” amesema Mwalimu huku akimwelezea Machemba kama kiongozi anayefaa kupewa nafasi.

Amewaasa wananchi kuachana na masihara na kumchagua mtu bora mwenye uwezo wa kuwatumikia kwa uadilifu na ufanisi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii