Lissu afikishwa mahakamani mapema leo

Leo Alhamisi Septemba 11 mwaka huu ni siku ya nne mfululizo ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam inaendelea kusikiliza mapingamizi ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu.

Wakati Mahakama inaendelea kusikiliza hoja za mshtakiwa kwenye mapingamizi hayo, leo akitarajiwa kujibu hoja zilizoibuliwa na upande wa Jamhuri unaopinga mapingamizi hayo tayari Tundu Lissu amewasili mahakamani hapo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii