MGOMBEA Mgombea ubunge wa jimbo la Muheza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamis Mwinjuma amesema iwapo atachaguliwa nafasi hiyo ataendelea kushughulikia changamoto za wananchi.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni yake iliyofanyika katika kata ya Misalai tarafa ya Amani wilayani humo ambapo amesema kuwa atahakikisha anashirikiana nao bega kwa bega katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zao.
Akitoa salama za Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman, Mjumbe wa Kamati wa Siasa ya Mkoa, Nassor Makau amewataka watia nia nafasi za ubunge na udiwani kufanya kampeni za kiustaarabu.
“Nendeni mkanadi sera zenu lakini na ilani ya chama kwani wananchi wanataka kusikia namna ambavyo mtashughulikia kero zao na sio kampeni za vurugu na maneno ya kashfa,”amesema Makau.