Rapa Fat Joe
amesema kuwa “Bifu” lake kubwa dhidi ya 50 Cents na Jay Z lililotokea katika
miaka ya 2000, lilimgharimu mabilioni ya fedha kitu ambacho hatokuja kukisahau
katika maisha yake.
Akizungumza
kupitia Podcast ya “Sneaker Shopping”, Fat Joe ambaye alikuwa ni kiongozi wa
TERROR SQUARD amesema kuwa, ugomvi huo baina yake na wasanii hao wawili
uliovuma kweli kweli, ulimfanya apoteze “Dili” la mabilioni ya fedha alilokuwa
amelipata kupitia chapa za AIR JORDAN na REEBOK.
Katika
maelezo yake, mkali huyo wa wa “Make It Rain” amefafanua kuwa, Michael Jordan
aliamua kusitisha kabisa dili lake na Fat Joe (Air Jordan) baada ya kutokea
sintofahamu na mvutano mkubwa baina yake (Fat Joe) dhidi ya 50 Cents katika
tuzo za MTV VMA’s zilizofanyika mwaka 2005.
“Michael
Jordan aliniita akaniambia, Fat Joe, mimi sio mtu wa migogoro na ugomvi. Jambo
letu tulitazame kipindi kijacho” alisema Fat Joe
Pia
alimalizia kwa Kusema kuwa, Kampuni ya Reebok iliahidi kupiga naye biashara ya
mabilioni ya fedha, lakini ilipogundua kuwa alikuwa na ugomvi na Jay Z, haraka
sana walisitisha dili hilo na kuyeyuka kwa staili hiyo