VIJANA WAHIMIZWA KUTUMIA FURSA MBALIMBALI ZILIZOPO KUEPUKA CHANGAMOTO YA KUJIUA

Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Baraka Makona ametoa wito kwa jamii kutumia fursa mbalimbali zilizopo ili kuondokana na changamoto ya watu kujiua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo changamoto za kiuchumi 

Makona ameyasema hayo katika warsha maalumu iliyoandaliwa na Taasisi ya Mothers Helping Mothers kwa kushirikiana na Soma kwa Furaha Initiative September 10 ambapo ni maathimisho ya siku ya kimataifa ya kuzuia vifo vya kujiua

Aidha kwa upande mwingine Stella Raphael ambae ni Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilemela amesisitiza wazazi kutoa malezi bora kwa watoto ambayo yatawajengea misingi na kuwa imara ili kukabiliana na changamoto za kimaisha zinazoweza kumpelekea mtu kujitoa uhai

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii