VIJIDUDU TUMBONI VINAVYOSIMAMIA USINGIZI HADI UADILIFU WA AFYA

Sasa, wanasayansi wanapanga kuwatumia, ili kusaidia kumletea mtu usingizi kitandani usiku, mwili wake utakuwa na shughuli nyingi.

Katika kila inchi ya mwili ndani yake kunatajwa kuwapo viumbe vidogo wanajongea na msongamano, wakigombea nafasi.

Utafiti unaonesha kuwa jamii za bakteria, virusi na fangasi walioko katika miili ya watu, wanaweza kuathiri usingizi wake mtu. Hapo ndio huathiri usingizi kuwa bora au kudhoofika.

Ni uelewa unaofungua njia mpya za kushughulikia matatizo ya usingizi na kuvurugika ratiba ya mwili kitaalamu inaitwa ‘circadian rhythms.’

Watu wengi kwa sasa hutegemea dawa maalum kudhibiti usingizi sugu, ila taaluma iendako, bakteria rafiki watatumika kusaidia watu kulala na kuleta maana mpya kwa dhana ya ’usingizi safi.’

"Kwa muda mrefu, dhana kuu imekuwa kwamba matatizo ya usingizi huvuruga microbiome (vijidudu) zetu," anasema Prof. Jennifer Martin, kutoka Chuo Kikuu cha California, Los Angeles, Marekani.

"Sasa kuna ushahidi unaonesha kwamba uhusiano huu huenda ni wa pande mbili," anaendelea mtaalamu  huyo, akifafanua mnamo Mei mwaka huu, utafiti mpya uliowasilishwa katika Kongamano la Wanasayansi wa Usingizi, ulichanganua namna usingizi huo ungefikiwa.

Utafiti pia unabainisha kuwa, wenye tatizo la usingizi lililothibitishwa kitaalamu. wana tofauti ya bakteria tumboni, ikilinganishwa na wanaolala vizuri.

Ni hali inayoashiria kinga dhaifu mwilini, katika uchakataji mafuta na sukari na inaweza kuongeza hatari ya kisukari, pia unene uliopitiliza, na maradhi ya moyo.

Utafiti mwingine uliowashirikisha watu 40 waliovaa vifaa vya kupima usingizi kwa mwezi mmoja, walibaini kwamba kutopata usingizi ulihusishwa na upungufu wa bakteria wa utumbo.

Watu waliokuwa na tofauti ya ratiba zao za usingizi kati ya siku za kazi na wikendi, walionekana kuwa tofauti sana na waliokuwa na ratiba thabiti ya usingizi kwa mujibu wa uchambuzi wa kampuni ya afya ya teknolojia ya nchini Uingereza.

"Hii inaweza kusababisha matatizo ya mmeng'enyo wa chakula na magonjwa ya kimetaboliki ambayo ni ya kawaida miongoni mwa wafanyakazi wa zamu, na microbiome iliyovurugika inaweza kuchangia hayo yote." anatamka Prof. Kenneth Wright kutoka Chuo Kikuu cha Colorado Boulder, Marekani.

Inawezekana pia watu wenye usingizi wa mang'amung'amu hufuata lishe duni, jambo linaloweza kuathiri microbiome zao, anasema Prof. Sarah Berry wa Chuo cha King's College London na mwanasayansi mkuu wa Zoe.

Anataja utafiti mwingine unaonesha kuwa watu wanaolala kwa muda mfupi huongeza ulaji wao wa sukari bila kujitambua.

"Sehemu ya nadharia ni kwamba ukipata usingizi wa mang'amung'amu, vituo vya ridhaa kwenye ubongo wako huongezeka shughuli, na hivyo unatafuta 'tiba ya haraka', akisema "Ubongo wako unakushawishi kutaka wanga rahisi ili upate nguvu za haraka."

Mabadiliko ya lishe yanatajwa si sehemu pekee ya tatizo. Prof. Berry na wenzake wakabaini, aina tisa za bakteria walioongezeka na nane waliopungua kwa watu wenye mishemishe nyingi kwa siku.

BAKTERIA WAHARIBIFU

Prof. Jaime Tartar wa Saikolojia na Neurosayansi kutoka Chuo Kikuu cha Nova Southeastern, Florida, Marekani, ambaye hakuhusika katika utafiti huo, anaeleza kushawishika kuwa baadhi ya bakteria huathiri moja kwa moja usingizi wao.

Analitaja kundi la Firmicutes, akirejea utafiti alioufanya kwa wanaume 40, akagundua makundi 15 tofauti ya wadudu hao, yaliyoonesha uhusiano na viwango vya usingizi.

"Hatuna majibu yote kwa sasa, lakini inaonekana kuwa baadhi huimarisha usingizi na mengine huuvuruga," anasema.

Baadhi ya mikasa ni ya usingizi usiotosha, unaweza kusababisha mabadiliko ya wadudu na kinga zao wadhoofisha kinga za mwili, jambo linaloleta matatizo ya usingizi kwa muda mrefu.

Watafiti kama Prof. Martin na Tartar, wanaamini baadhi ya matatizo ya usingizi, yanasababishwa na kukosa usawa wa bakteria tumboni au mdomoni.

Anaeleza kuwa bakteria huathiri ubora wa usingizi kwa kuingilia midundo ya mwili na kudhibiti kiwango cha ulaji chakula, mambo yote yanahusiana na usingizi wa mtu.

Ni ushahidi unaotokana na mfululizo wa tafiti. Mmojawapo mwaka 2024, wanasayansi walipandikiza kinyesi chenye bakteria kutoka kwa binadamu kwenda kwa panya.

Panya nao wakapokea kinyesi kutoka kwa watu wenye shughuli nyingi kwa siku na wanaokosa usingizi, walionyesha tabia za kukosa usingizi, wakibaki macho katika saa zao za kawaida za kulala.

Utafiti mwingine, panya waliopokea bakteria kutoka kwa binadamu katika awamu mbalimbali za shughuli, wakaonesha ongezeko la uzito na matatizo ya kudhibiti sukari.

Tafiti ndogo kutoka China, zinaonesha upandikizaji wa kinyesi, unasaidia wagonjwa wenye matatizo sugu ya usingizi. Hata hivyo, wanagusa, uafiti unahitajika kuthibitisha matokeo hayo.

LISHE NA USINGIZI

Kuna wanaume 15 walipopewa lishe yenye mafuta na sukari nyingi kwa wiki, walionesha mabadiliko katika umeme wao wa ubongo wakiwa usingizi mzito.

Vilevile, utafiti mwingine uliohusisha watu waliotumia antibaiotiki, ulionyesha kupungua usingizi, katika kipindi muhimu mwili hujijenga upya na kuimarisha kumbukumbu, ingawa matokeo hayakuhusu aina zote za antibaiotiki.

Inajulikana, bakteria wa utumbo huzalisha mahitaji kama asidi, yote vina nafasi katika usingizi. Inatajwa, viumbe hao wanapopungua, athari zao kwenye ubongo hupungua.

"Vijidudu hai mwilini havina uwiano. Hali hiyo inaweza kusababisha uvimbe wa ndani na wa mwili mzima, jambo linaloweza kusababisha njia ya hewa kuwa nyembamba.

“Kuongezeka kwa homoni za msongo wa mawazo, pamoja na athari nyingine nyingi zinazoweza kuvuruga usingizi kwa muda mrefu," anasema Prof. Martin.

Njia ya hewa inapozibwa au kupungua upana wake, inatajwa kusababisha matatizo kama vile kuzuiwa usingizi na kukoroma.

TIBA INAYOPENDEKEZWA

Tiba iliyopendekezwa na Prof. Martin. Ni kwamba anavutiwa na matokeo hayo, akisisitiza umuhimu wa tafiti kubwa

Anasema:"Katika taaluma ya tiba ya usingizi, tunakabiliana na changamoto kubwa ya kuwasaidia watu hawa, wengi wao wakiwa hawapendi kutumia dawa zinazowalaza."

Lakini iwapo sayansi ya vijidudu vidogo itathibitika kuwa na athari ya moja kwa moja kwa ubora wa usingizi, basi hiyo inaweza kuwa habari njema kwa watu wa aina mbalimbali.

"Uvunjifu wa mdundo wa moyo ni jambo la kawaida sana katika jamii ya sasa," anasema Prof. Wright.

Kwa mujibu wa taarifa za kiafya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii