WAAJIRIWA WAPYA WIZARA YA ARDHI WAHIMIZWA KUJIEPUSHA NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amewasisitiza watumishi wa ajira mpya wa wizara hiyo kufuata maadili ya utumishi wa umma na kujiepusha na tabia ya unyanyasaji wa kijinsia katika vituo vya kazi walivyopangiwa. 

Mhandisi Sanga amesema hayo Septemba 22 mwaka huu katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya awali kwa Maafisa Ardhi, Maafisa Usajili Wasaidizi, Wabunifu Majengo na Wakufunzi watakaofundisha katika Chuo cha Ardhi Tabora.

“Kwenye suala la unyanyasaji wa kijinsia msikae kimya, likitokea, toeni taarifa kwa mamlaka za Wizara. Jambo hili tunalichukulia kwa umuhimu wake, mnaweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja” amesisitiza Mhandisi Sanga.

Katika miezi ya hivi karibuni, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepokea takriban watumishi wa ajira mpya 400 ambao wamepangiwa kufanya kazi katika mikoa mbalimbali nchini ambapo natarahisisha utoaji huduma kwa wakati katika sekta ya ardhi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii