Katibu Mkuu wizara ya Maji aweka kambi Butimba kurejesha huduma ya maji

Katibu Mkuu Maji aweka kambi Butimba kwa saa 24 kuhakikisha huduma ya maji inarejea Mwanza.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefika katika mradi wa maji wa Butimba kufuatilia marekebisho yanayoendelea ili kurejesha huduma ya maji katika hali ya kawaida kutokana na  hitilafu iliyotokea katika  mtambo wa kusukuma maji. 

Mhandisi Mwajuma amefanya kazi kwa saa 24 na wataalam katika kurekebisha hitilafu iliyojitokeza kwa lengo la  kuhakikisha maji yanapatikana kwa wananchi muda wote kutokana na  uwekezaji mkubwa wa serikali katika mradi wa maji wa Butimba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii