Mwanza huduma ya maji yarejea kwa baadhi ya maeneo

Huduma ya maji imeanza kurejea katika baadhi ya maeneo yaliyokua yameathirika kwa kukosa huduma ikiwemo Nyegezi, Mkolani, Stendi ya Mabasi Nyegezi, Kuzenza, Nyabulogoya, Iseni, Luchelele, Igubinya, Sweya, Kijiweni na maeneo jirani.

Maeneo hayo yameanza kupata maji kufuatia kukamilika kwa kazi ya uungaji wa bomba la usafirishaji maji eneo la Mkuyuni lililoungwa kama mpango mbadala wa kuwezesha maji kutoka chanzo cha Capripoint kuhudumia maeneo yaliyoathirika, wakati matengenezo makubwa yakiendelea chanzo cha Butimba.

Aidha, Wataalam na Mafundi wa MWAUWASA wapo mtaani kufuatilia maendeleo ya upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo yaliyokua yameathirika.

Huduma ya maji itaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na maji yanavyosafiri.

MWAUWASA inaendelea kuwashukuru Wananchi kwa uvumilivu na inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa maboresho haya.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii