Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za vivuko kote nchini, kwa kujenga vivuko vipya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma iliyo bora.
Picha ni Kivuko cha MV Bukondo ambacho kinakwenda kutoa huduma kati ya Bwiro na Bukondo Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, eneo ambalo halijawahi kuwa na kivuko hapo awali.
Kina uwezo wa kubeba abiria 200, magari 10 sawa na tani 100, kimegharimu shilingi Bilioni 4.5 na kinakwenda kuchochea shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.