MKUTANO WA 20 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA UTAMADUNI NA MICHEZO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA DAR ES SALAAM SEPTEMBA 23 MWAKA HUU.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) amemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo katika Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Elimu Sayansi na Teknolojia Utamaduni na Michezo uliofanyika Dar es Salaam Septemba 23 mwaka huu.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri mbalimbali kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na viongozi wengine mbalimbali ikiwemo Makatabu Wakuu na Wakuu wa Taasisi za Elimu za EAC ukiwa na ajenda mahususi ya kujadili masuala anuai yanayogusa Sekta ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Sanaa na Michezo.
Mhe. Londo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo huku akiambatana na viongozi wengine ikiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa